Tuesday, April 26, 2016

WENGER ANGALIA HII

MASHABIKI WA ARSENAL WAKISISITIZA KWAMBA WAKATI WA WENGER KUONDOKA NDIYO HUU

GOOD KISS IN PITCH [ONUOHA VS RAKELS]



Beki Nedum Onuoha wa QPR (kushoto) akipambana na Deniss Rakels wa Reading katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza England kwenye Uwanja wa Loftus Road, juzi. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya mabao 1-1. Hapa kila mmoja alikuwa akiwania mpira, akajikuta amempa mwenzake “busu”.

sources;salehjembe

VARDY KUWAKOSA MAN U KWA KUONGEZEWA ADHABU


Mshambuliaji Jamie Vardy atakosa mechi moja zaidi ya Leicester City.

Mechi inayofuata ni dhidi ya Manchester United, adhabu ambayo anaipata baada ya kumfokea mwamuzi aliyemlamba kadi.

Kamati ya Sheria ya FA, yenye watu watatu imepitsha hilo.


Hii itakuwa ni mechi ya pili Leicester inacheza bila ya Vardy. Mechi iliyopita iliitwanga Swansea kwa mabao 4-0 mchezaji huyo akiwa jukwaani na mpenzi wake.

MANENO YA BLUE DHIDI YA SUGU BAADA YA KUCHUKULIWA NYIMBO YAKE NA SUGU




  • mrbluebyser1988Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli ..!! SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia ..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa "Freedom" tulifanya pale kwa makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia..sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn...mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu....????

maneno hayo ameandika kwenye page yake ya instagram ya blue

JUVENTUS BINGWA MARA YA TANO MFULULIZO

Juve-bingwa
Juventus imeshinda taji la Serie A kwa mara ya tano mfululizo!
Ushindi wa bao 1-0 ilioupata Roma dhidi ya Napoli leo umeipa ubingwa wa Scudetto timu ya Juventus.
Juventus ilanza vibaya msimu wa 2015-26 baada ya msimu uliopita kunyakua mataji mawili na kufika hatua ya fainali ya Champions League na kupoteza mbele ya Barcelona.
Wakiwa bila ya nyota wao Andrea Pirlo na Carlos Tevez haikuwa rahisi kwao kufanya vizuri na hilo lilithibitika mwanzoni mwa msimu kabla ya kukaa sawa.
Kikosi hicho kilicho chini ya Massimo Allegri kilizinduka na kuanza kuikimbiza Napoli iliyokuwa kwenye kiwango bora mwanzoni mwa msimu, Juve waliipiga bao Napoli wiki chache zilizopita na kufanikiwa kutetea ubingwa wao.

SPURS WA DRAW SASA LEICESTER BADO POINT 3 KUWA MABINGWA WA EPL

Mchezaji mpya bora chipukizi wa Mwaka wa Ligi Kuu ya England, Dele Alli wa Tottenham Hotspur akipasua katikati ya wachezaji wa West Bromwich Albion katika mchezo wa ligi hiyo usiku wa Jumatatu Uwanja wa White Hart Lane, London. Timu hizo zimetoka sare ya 1-1, Craig Dawson akianza kujifunga dakika ya 33 yeye mwenyewe kuisawazishia West Brom dakika ya 73