Tuesday, April 26, 2016

JUVENTUS BINGWA MARA YA TANO MFULULIZO

Juve-bingwa
Juventus imeshinda taji la Serie A kwa mara ya tano mfululizo!
Ushindi wa bao 1-0 ilioupata Roma dhidi ya Napoli leo umeipa ubingwa wa Scudetto timu ya Juventus.
Juventus ilanza vibaya msimu wa 2015-26 baada ya msimu uliopita kunyakua mataji mawili na kufika hatua ya fainali ya Champions League na kupoteza mbele ya Barcelona.
Wakiwa bila ya nyota wao Andrea Pirlo na Carlos Tevez haikuwa rahisi kwao kufanya vizuri na hilo lilithibitika mwanzoni mwa msimu kabla ya kukaa sawa.
Kikosi hicho kilicho chini ya Massimo Allegri kilizinduka na kuanza kuikimbiza Napoli iliyokuwa kwenye kiwango bora mwanzoni mwa msimu, Juve waliipiga bao Napoli wiki chache zilizopita na kufanikiwa kutetea ubingwa wao.

No comments:

Post a Comment