Thursday, April 28, 2016

DIEGO SIMEONE KAFUNGIWA MECHI ZOTE KUWA JUKWAANI


KOCHA Mkuu wa Atletico Madrid, Diego Simeone(pichani kulia)amefungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi zote tatu zilizobaki za timu yake katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga kumalizia msimu.
Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 45 amepewa adhabu hiyo baada ya mpira kurushwa uwanjani katika mchezo wa Jumamosi, timu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Malaga.
Picha za Televisheni zinaonyesha kwamba mpira huo ulipokuwa nje katika himaya ya kijana muokota mpira, ukarushwa uwanjani kutoka eneo la benchi la Atletico Madrid na kuvuruga shambulizi la Malaga. 
Na kwa kuwa mpira uliporushwa kutoka eneo la benchi la ufundi la Atletico - sheria zinambana kocha kwamba ndiye wa kuwajibishwa na Simeone amedhibiwa. 
Kocha huyo wa Atletico alipandishwa jukwaani na refa Antonio Mateu Lahoz baada ya ripoti kusema hakumtaja aliyerusha mpira uwanjani.
Madrid inalingana kwa pointi Barcelona kileleni mwa msimamo wa La Liga, wakati Real Madrid inazidiwa pointi moja katika nafasi ya tatu.
Simeone sasa hatakaa benchi katika mechi dhidi ya Rayo Vallecano, Levante na Celta Vigo.

MAAJABU YA WAKALI WANAO VAA NO 7

Nomber 7
Suala la wachezaji kuvaa jezi namba flani mgongoni mara nyingi huwa linaongozwa na imani, hii hapa ni list ya wachezaji saba ambao wamewahi kufanya mambo makubwa kwenye soka wakiwa wamevaa jezi namba 7 mgongoni.
7. Robert Pires
Pirez
Robert Pires alidumu kwenye kikosi cha Arsenal kwa miaka 6 pekee lakini ilitosha heshima kwenye klabu hiyo na kuwa miongoni mwa wachezaji wa kukumbukwa kwenye historia ya Arenal.
Baada ya mafanikio makubwa kwenye michuano ya kombe la dunia na Euro mwaka 1998 na 2000 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, Pires alijiunga na The Gunners na kukiongoza kikosi hicho kutwaa kombe makombe matatu ya FA na mataji mawili ya Premier League.
Kutokana na mchango wake kwenye kikosi cha Arsenal katika miaka 6 aliyoitumikia, alichaguliwa na mashabiki kama mchezaji wa sita mwenye mchango mkubwa kwenye timu.
6. Luis Figo
Figo
Nahodha wa aina yake kuwahi kutokea kwenye timu ya taifa ya Ureno ambaye alikuwa akivaa jezi namba 7 na kupata mafanikio makubwa. Winga mwenye uwezo wa juu kipindi cha uchezaji wake, anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kukimbia na mpira huku akiwaacha mabeki huku akiwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake kufunga.
Nyota huyo wa Ureno atakumbukwa wakati anakitumikia kikosi cha Inetr Milan na Real Madrid licha ya kushindwa kutwaa taji lolote akiwa na timu yake ya taifa lakini anabakia kuwa miongoni wachezaji bora kuwahi kutokea Ureno.
5. George Best
Best
George Best ni nyota mwingine wa Manchester United, alithibitisha jina lake kwa uwezo wake uwanjani katika miaka yote aliyocheza soka.
Mu-Ireland huyo alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati na winger, alikuwa kwenye kiwango bora kati ya 1966-72 ambapo aliiongoza United kutwaa mataji ndani na nje ya England huku akifanikiwa kushinda tuzo binafsi.
4. Kenny Danglish
Dalgrish
Kenny Danglish alikuwa ni miongoni mwa wachezaji muhimu ndani ya Liverpool kwenye miaka ya 1970 na 80 na anatambuliwa kama miongoni ya wachezaji bora kuwahi kuitumikia Liverpool.
Alichukua namba 7 ambayo ilikuwa inavaliwa na mkongwe mwingi wa Liverpool Kevin Keegan, lakini alifanikiwa kupata mafanikio kuliko alyemtangulia kuvaa jezi hiyo.
3. Eric Cantona
Cantona
Akiwa anatambulika kwa a.k.a ya ‘Premier League bad boy’, Eric Cantona ni miongoni mwa majina yenye heshima kuwahi kuvaa jezi namba 7 ya United.
Licha ya kuchukiwa na baadhi ya mashabiki, Cantona alifanikiwa kuwateka mashabiki wengi wa United kutokana na kiwa alichokuwa anakionesha uwanjani. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alidumu United kwa miaka 5 lakini aliweza kufunga magoli 80 na kushinda mataji kibao ikiwemo ya mataji matatu (treble) ya mwaka 1999.
2. Garrincha
Garrincha
Garrincha ni jina maarufu kwenye soka la Brazil, anasimama kama mchezaji bora kuwahi kutokea amabaye alikuwa akivaa jezi namba 7. Akiwa amekiongoza kikosi cha Seleccao kutwaa kombe la dunia mwaka 1972 bila ya Pele. Garrincha alikuwa pia nyota wa klabu ya Botafogo.
Legend huyo wa Brazil alichaguliwa kwenye timu ya karne ya 20 na timu ya FIFA ya muda wote ya kombe la dunia.
1. Cristiano Ronaldo
FC Bayern Muenchen v Real Madrid - UEFA Champions League Semi Final
Star wa Real Madrid anafunga list hii ya wachezaji waliowahi kupata mafanikio wakiwa ndani ya jezi namba 7 huku akiwa bado na muda wa kuendelea kufanya makubwa zaidi.
Akianza kupata mafanikio kwenye klabu ya Manchester United, mreno huyo mwenye kipaji cha aina yake alihamia Hispania mwaka 2009 na ameendelea rekodi ya kufunga magoli ambayo itawachukua muda mrefu ma-striker kuivunja.
Lakini Ronaldo bado hajashinda taji lolote akiwa mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno, mambo yote hayo makubwa ambayo Ronaldo ameyafanya kwenye soka akiwa amevaa jezi namba 7.

SOURCES;SHAFFIH DAUDA

ATLETICO WAICHAPA BAYERM MUNICH



MATCH FACTS

Atletico Madrid (4-4-2):

 Oblak 7; Juanfran 7, Gimenez 7, Savic 7, Luis 6.5; Saul 8 (Teye 85mins), 

Gabi 7.5, Fernandez 7, Koke 6.5; Griezmann 6.5, Torres 7.

Unused subs: Correa, Gamez, Hernandez, Kranevitter, Moya, Vietto.

Booked: Saul.

Goal: Saul 11.

Manager: Diego Simeone 8.

Bayern Munich (4-1-4-1):

 Neuer 6; Lahm 6, Martinez 6, Alaba 5.5, Bernat 5.5 (Benatia 77); Alonso 6; 

Costa 6.5, Alcantara 5 (Muller 70, 6), Vidal 6.5, Coman 6 (Ribery 64, 6); Lewandowski 6.

Unused subs: Gotze, Kimmich, Tasci, Ulreich.

Booked: Costa, Benatia, Neuer.

Manager: Pep Guardiola 6.

Referee: Mark Clattenburg 7.

Saul was joined by his jubilant Atletico team-mates after his goal set up a 1-0 first leg advantage for the Spanish side

Vidal gets to the ball ahead of Gabi in the midfield battle as Bayern battled to wrestle back Atletico's early advantage in the game
Lewandowski and Vidal found opportunities scarce at the Vicente Calderon before Muller was brought on to join the attack