Tuesday, April 19, 2016

KIKOSI BORA CHA FABREGAS EPL 2015/2016 NI LEICESTER NA SPURS



“Siyo kazi rahisi kuchagua hasa katika safu ya mlinda mlango, Kasper Schmeichel amefanya kazi nzuri na anastahili kuwemo katika kikosi hiki lakini De Gea ameokoa pointi nyingi za Man Utd. Mungu mwenyewe anajua ni pointi ngapi,” alisema Fabregas.

Kikosi kizima cha Fabregas kinasomeka hivi:


1. David de Gea
2. Hector Bellerin
3. Toby Alderweireld
4. Robert Huth
5. Ryan Bertrand
6. Riyad Mahrez
7. N'Golo Kante
8. Dele Alli
9. Dimitri Payet
10. Jamie Vardy
11. Harry Kane  

RONALDO KUHAMIA PSG?

Headlines za staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid yaHispania Cristiano Ronaldo kuhusishwa kutaka kuhama Real Madrid na kutaka kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa zimerudi tena katika mitandao.
Awali Ronaldo aliwahi kuhusishwa kutaka kujiunga na PSG ila leo April 19 2016 stori kutoka 101greatgoals.com wameripoti kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi mara tano, stori zinaeleza kuwa Jose Mourinhohuenda akajiunga na PSG pamoja na Ronaldo msimu ujao.
Taarifa za Ronaldo kukutana na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi zimevuja baada yaRonaldo kudaiwa kuonekana akiwa Paris Ufaransa kwa ndege ya kukodi na kupelekwa katika hoteli aliyopo Nasser Al-Khelaifi na siku inayofuatia Ronaldo anadaiwa kuondoka na ndege binafsi tena kuwahi mazoezi ya Real Madrid. Huenda kukawa kuna kitu kinaendelea kwani Ronaldo amekuwa akionekana Paris mara kadhaa sasa.

SPURS YAIFUNGA STOKE CITY

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (kushoto) akishangilia na Jan Vertonghen baada ya kuifungia mabao mawili timu yake katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Britannia. Mabao mengine ya Spurs yalifungwa na Dele Alli na sasa timu hiyo inafikisha pointi 68 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kukaa nafasi ya pili nyuma ya Leicester City yenye pointi 73 za mechi 34 

MAN UNITED YAZIFUNIKA BARCELONA,REAL MADRID

 Jarida la Forbes linalodili na masuala ya biashara na fedha limechapisha listi ya vilabu 10 vilivyoingiza faida kubwa duniani kote.
   Pamoja na matokeo yasiyoridhisha uwanjani, klabu ya Manchester United imetajwa na jarida la Forbes la Marekani kuwa klabu iliyoingiza faida kubwa zaidi kwa miezi 12 iliyopita. 
Listi kamili ya vilabu 10 vya soka vyenye faida kubwa.
1. Manchester United: $190 million
2. Real Madrid: $162 million
3. Manchester City: $131 million
4. Arsenal: $122 million
5. Liverpool: $115 million
6. Barcelona: $108 million
7. Juventus: $81 million
8. Tottenham Hotspur: $73 million
9. Schalke: $67 million
10. Bayern Munich: $60 million