Thursday, April 21, 2016

PFA TEAM OF THE YEAR ,OZIL AYUPO

Kikosi hicho ambacho kimetajwa na Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) hakijataja jina la Ozil kama wengi alivyokuwa wakimtegemea huku chipukizi wengine wakitajwa kuwa ndiyo wanaounda kikosi hicho.

Baadhi ya chipukizi waliotajwa katika safu ya kiungo ya kikosi hico ni Dimitri Payet, N'Golo Kante, Dele Alli na Riyad Mahrez.


MAN UNITED LIVERPOOL ZASHINDA EPL.....

Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney (kulia), akiwania mpira dhidi ya Lee Chung-yong wa Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Old Trafford. United imeshinda 2-0, mabao yake yakifungwa na Damien Delaney aliyejifunga dakika ya nne na Matteo Darmian dak55.


Mshambuliaji wa Liverpool, Divock Origi (kulia) akiwa juu kuwania mpira dhidi ya beki wa Everton, Ramiro Funes Mori aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 50 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield. Liverpool imeshinda 4-0, mabao yake yakifungwa na Origi dakika ya 43, M. Sakho dakika ya 45 na ushei, Daniel Sturridge dakika ya 61 na Philippe Coutinho dakika ya 76

KATI YA HAWA MASTRIKER WA ENGLAND YUPI ANAENDA EURO FRANCE

MAGNIFICENT7_2809770al

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson anaelekea kuwa na wakati mgumu kuchagua washambuliaji watakaoisaidia timu hiyo kwenye michuano ya Uero mwaka huu nchini Ufaransa.
MAGNIFICENT7_2809770al
Mpaka sasa Hodgson ana chaguo la wachezaji saba ambapo anatakiwa achague wachezaji wanne au watano kati yao.
Hawa ni washambuliaji wanaomuumiza kichwa Hodgson kufanya uchaguzi yupi atakayeshiriki michuano ya Uero 2016.
Harry Kane
2E3EB91900000578-0-image-a-82_1447074705638
Kane ndiyo mchezaji anayeongoza kwa ufungaji kwenye ligi ya Uingereza akiwa ameshafunga magoli 24. Mpaka sasa anaonekana kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza wateuliwa na Hodgson kwenye timu ya Uingereza kushiriki michuano ya Uero.
Games 34
Games started 34
Mins played 3,008
Assists 1
Goals 24
Chances created 41
Goals/game 0.71
Win rate 56%
Jamie Vardy
Leicester-Citys-English-striker-Jamie-Vardy-celebrates
Nyota huyu amesaidia Leicester City kushika usukani wa kuongoza ligi ya Uingereza kwa pointi 73. Vardy ameshafanikiwa kufunga magoli 22 akishika nafasi ya pili nyuma ya Harry Kane wa Tottenham.
Games 34
Games started 34
Mins played 2,959
Assists 6
Goals 22
Chances created 47
Goals/game 0.65
Win rate 62%
Wayne Rooney
wayne555_2809708al
Rooney ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na tayari anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye timu ya taifa akifunga magoli 51. Japo kwa msimu huu anaonekana kutofanya vizuri sana kwenye timu yake ya Manchester United na majeraha yaliyomuandama ambayo yalimfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda kidogo.
Games 23
Games started 22
Mins played 1,972
Assists 4
Goals 7
Chances created 34
Goals/game 0.30
Win rate 44%
Daniel Sturridge
JS44222832
Japo kipindi cha nyuma alionekana kutofanya vizuri kwenye timu ya Liverpool, Sturridge kwa sasa ameonekana kuwa ni mmoja wa washambuliaji muhimu kwenye timu hiyo. Kwa muda mrefu hakuwepo kwenye timu ya taifa ya Uingereza kwa sababu ya kupata majeraha yaliyomfanya aweze kukaa nje wa muda mrefu.
Games 10
Games started 8
Mins played 673
Assists 1
Goals 6
Chances created 4
Goals/game 0.60
Win rate 50%
Danny Welbeck
Welbeck
Welbeck ni mmoja kati ya washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kurudi nyuma na kukaba wakati timu inashambuliwa. Japo amekuwa hayupo fiti kwa muda mrefu kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa majeraha ya muda mrefu, kwa sasa Welbeck ameonekana kurudi na kuanza kufanya vizuri ingawa ameonekana hapati nafasi sana kwenye timu ya Arsenal.
Games 8
Games started 6
Mins played 501
Assists 2
Goals 3
Chances created 5
Goals/game 0.38
Win rate 38%
Andy Carroll
Carroll
Kwa sasa Carroll ameonekana kuanza kurudi kwenye makali yake kama kipindi yupo timu ya Newcastle United kabla ya kuhamia Liverpool na kiwango chake kupotea. Hatrick yake kwenye mechi ya West Ham United dhidi ya Arsenal inamfanya Hodgson ajiulize mara mbili na kufikiria kuchanga karata yake vizuri.
Games 22
Games started 8
Mins played 1,010
Assists 1
Goals 8
Chances created 8
Goals/game 0.36
Win rate 41%
Marcus Rashford
Manchester-United-v-Midtjylland-Europa-League-Round-of-32-Second-Leg
Rashford amekuwa ni mmoja kati ya washambuliaji chipukizi wenye uwezo mkubwa wa kufunga magoli mazuri. Mpaka sasa Rashford ana umri wa miaka 18 ameonekana kuwa ni mmoja kati ya wachezaji tegemezi wa timu hiyo akiwa tayari kashafunga magoli 8 kwenye mashindano yote aliyoichezea timu ya Manchester United.
Games 7
Games started 7
Mins played 546
Assists1
Goals 4
Chances created 2
Goals/game 0.57
Win rate 71%

BEN POL AWA BABA KIMYA KIMYA

Ben

MSAnii wa kizazi kipya ben pol amepata mtoto wa kiume na kuwa baba lakini mwenyewe akuwai kupost kwenye mitandao ya kijamii lakini imekuja kuvuja baada ya mama wa mtoto huyo miss Tanzania no 2 Latifa mohamed kupost picha insta akiwa n mtoto huyo'
hongera bwana benard paul

MANUEL NEUR AFANYA HILI KWA BAYERN MUNICH


Habari nzuri kwa mashabiki wa Bayern Munich, Manuel Neuer ni kuwa kipa wao wamesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo mpaka mwaka 2021.

Neuer, 30, alijiunga klabuni hapo akitoka Schalke kwa euro milioni 30 mwaka 2011 na tangu hapo ameshinda mataji matatu ya Bundesliga na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2013.

Kipa huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani alikuwa akihusishwa kuwaniwa na Manchester City, klabu ambayo kocha wake wa sasa, Pep Guardiola atatua msimu ujao.




Inaelezwa kuwa mkataba huo wa sasa utamwezesha kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri kikosini hapo akiwa sawa na mshambuliaji Thomas Muller ambaye analipwa euro milioni 15 kwa mwaka.

Mkataba uliokuwepo kabla ya huo wa sasa wa Neuer ulikuwa ukimalizika mwaka 2019.