Friday, April 22, 2016

SIKIA MANENO YA FABREGAS


“Kuna wakati baada ya mechi dhidi ya Bournemouth nilikuwa nimelala kitandani, nilikuwa na masikitiko sana na kilichokuwa kikiendelea klabuni, nikamwambia mke wangu kuwa nimesahau hata jinsi ya kucheza mpira,” alisema Fabregas alipokuwa akizungumzia suala hilo kisha akaendelea:

"Sikuwa mimi, nilikuwa niponipo tu, ilifikia hatua ninampira lakini sijui niufanyie nini na sijui nimpasie nani.

"Hiyo miezi miwili au mitatu nilipoteza kabisa hali ya kujiamini.”


  Baada ya kuondoka kwa Mourinho kutokana na matokeo mabaya, angalau Chelsea ilianza kupata nafuu ya kupata matokeo ikiwa chini ya kocha wa muda Guus Hiddink tangu Desemba, mwaka jana.

"Nashukuru Mungu kila kitu kilienda vizuri na kubadilika na nikawa nacheza vizuri."

Licha ya matokeo mazuri kiasi bado mwendo wa timu hiyo haikuwa bora kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo mpaka sasa inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa Premier League.

SANCHEZ AIPAISHA ARSENAL

Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez akishangilia na beki wa kushoto, Nacho Monreal baada ya kuifungia timu yake mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Alhamisi Uwanja wa Emirates