Tomas Pina (kushoto) wa Villarreal akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Philippe Coutinho wa Liverpool katika Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League usiku huu Uwanja wa El Madrigal, Villarreal nchini Hispania. Villarreal imeshinda 1-0, bao pekee la Adrian Lopez dakika ya 92
Friday, April 29, 2016
SAKHO AFUNGIWA TENA

April 23 2016 uongozi wa klabu ya Liverpool ulitangaza kumsimamisha beki wa kati wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu hiyo Mamadou Sakho kutokana na kugundulika kutumia dawa za kusisimua misuli michezo, dawa ambazo ni kinyume na taratibu.
Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) leo limetangaza uamuzi au adhabu ya kumsimamisha Mamodou Sakho kwa siku 30, uamuzi ambao ni wa muda ili kuipa nafasi kamati ya maadili ya UEFA hadi itakapokaa na kutangaza adhabu rasmi.
Sakho ambaye alikuwa anachunguzwa na UEFA toka March 17 baada ya mchezo waEuropa league kati ya Man United dhidi ya Liverpool Old Trafford, amegundulika kutumia ‘Fat Burner’ kwa ajili ya kusisimua misuli, Mamadou Sakho atakumbana na adhabu kutoka UEFA baada ya kamati ya maadili kukaa na kuamua adhabu.
SOURCE;MILLARD AYO
MAMBO BADO KWA RONALDO

Jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid yaHispania Cristiano Ronaldo limerudi tena kwenye headlines leo Alhamisi ya April 28 2016. Ronaldo amerudi kwenye headlines baada ya Real Madrid kudaiwa kutoa ripoti ya maendeleo ya majeruhi yake.
Ronaldo ambaye amekosa mechi mbili za Real Madrid huenda akakosa michezo mingine ikiwemo mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City utakaochezwa Santiago Bernabeu, Ronaldo anadaiwa kupimwa na MRI Scan na kukutwa ana tatizo la msuli (muscle tear).
Subscribe to:
Posts (Atom)