Sunday, May 01, 2016
KUMBE MUME WA TIWA SAVAGE NDIO MZINGUAJI

Jamaa huyo alionesha nia ya kutaka kujiua kutokana na masahibu hayo. Hiyo ilipelekea jamii kubwa ya Nigeria imchukie Tiwa kwa kumuona kama mwanamke katili na anayemtesa mumewe. Lakini upande wa pili wa shilingi wa mkasa huo unaweza ukabadili mawazo yako.
Kwa mujibu wa Tiwa, mume wake ndiye mzinguaji mkubwa na ana vimbwanga haswaa.
Akiongea kwenye exclusive interview na Pulse TV, Tiwa alisimulia jinsi ambavyo mume wake alikuwa akimfanyia ikiwa pamoja na kumtelekeza kwa kutotaka kujua chochote pale alipolazwa hospitali nchini Jamaica alikoenda kufanya video na Busy Signal.
Anasema wakati anajiandaa kwenda kushoot, alianza kutoka damu nyingi ukeni kiasi cha kupoteza fahamu. Alimpigia simu na kumtumia ujumbe mumewe ikiwa pamoja na kumtumia picha akiwa hoi kitandani lakini hakujibiwa hadi anatoka hospitali.
Siku amerejea Nigeria na akiwa amelala usiku wa saa nane, simu ya mumewe iliita kwa namba iliyohifadhiwa kwa jina la biashara lakini alishangaa iweje kampuni impigie usiku huo. Anadai alichukua simu ya mumewe na kuanza kusoma ujumbe wa WhatsApp na ndipo alipogundua kuwa huyo alikuwa ni mwanamke na maongezi yao yalionesha kuwa walikutana hotelini na kufanya mapenzi. Kutokana na kitendo hicho aliondoka na kwenda kwa rafiki yake.
Anadai kuwa amekuwa akificha kwa muda mrefu kuhusu mume wake, lakini amedai tangu mtoto wao azaliwa, hajawahi kutumia hata senti kwaajili ya familia yao kwamba Tiwa ndiye kila kitu.
Amesimulia pia jinsi ambavyo mume wake amekuwa na tabia ya kumzunguka kwenye malipo ya show zake ambapo ametolea mfano wa harusi aliyotakiwa kwenda kutumbuiza London. Anasema alibaini kuwa mumewe alilipwa gharama zote lakini hadi anaenda kutumbuiza alimueleza kuwa hakuwa amelipwa. Kwakuwa alikuwa anafahamiana na miongoni mwa waandaji wa harusi hiyo alimuuliza na kujibiwa kuwa walikuwa wameshamlipa mume wake hela yote, miezi minne nyuma.
“Unamuibia mke wako, na yeye haoni kama ameniibia mimi, kwahiyo ilibidi nitumbuize kwenye harusi bure, kwasababu alikuwa ameshatapeli hela na sijui alizifanyia nini,” anasimulia.
Kwa upande mwingine staa huyo alieleza jinsi ambavyo mume wake alikuwa akiishia maisha ya zaidi ya kipato chake na hivyo wakati mwingine kumfanya ajikute kwenye madeni makubwa ambayo alilazimika kuyalipa.
Tiwa anasema jambo ambalo mume wake alizingua zaidi na ambalo limesababisha mgogoro wao ni pale alikopa naira milioni 45 ambazo ni sawa na shilingi milioni 495 za Kitanzania na kuchikichia. Kwa hali hiyo Tiwa alianza kuhofia usalama wake kwamba wanaomdai mumewe wangeweza hata kumdhuru ama kumteka yeye na mwanae kwasababu ya deni hilo.
Pia Tiwa amezungumzia jinsi ambavyo aligundua mume wake anatumia cocaine kitu ambacho kilimuumiza sana.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alikanusha kwa msisitizo kuwa hajawahi kamwe kumsaliti mume wake na Don Jazzy, Dr Sid wala 2Face na kwamba yupo tayari hata kuwekewa kifaa cha kubaini kama anasema uongo.
Mpaka hapo Tiwa ameonesha nia ya kuachana na mume wake, kitu ambacho anadai hakupenda kiwe.
SOURCE;BONGO5
KIKOSI CHA SIMBA KINACHOOANZA LEO DHIDI YA AZAM
Kikosi cha Simba dhidi ya Azam FC leo...
1. Vincent Agban
2. Emery Nimuboma
3. Mohammed Tshabalala
4. Juuko Murshid
5. Novart Lufunga
6. Justise Majabvi
7. Awadh Juma
8. Jonas Mkude
9. Hamis Kiiza
10. Danny Lyanga
11. Peter Mwalyanzi
BENCHI:
Peter Manyika
Mohammed Fakhi
Hassan Ishaka
Brian Majwega
Mussa Mgosi
Raphael Kiongera
Hijja Ugando
sources;salehjembe
SIMBA VS AZAM NANI KUWA MBABE
NYASI za Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo zinatarajiwa kuwaka moto kwa mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC na Simba.
Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 58 na Simba 57 katika nafasi ya tatu, kwa pamoja zinaifukuzia Yanga katika mbio hizo za ubingwa, ambayo ipo kileleni baada ya kufikisha jumla ya pointi 65 kufuatia ushindi wa jana wa 2-1 dhidi ya Toto Africans mjini Mwanza.
Mabingwa hao wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Kagame Cup) imefanya maandalizi ya nguvu kukabiliana na Wekundu hao, ambao wenyewe walienda kujichimbia visiwani Zanzibar kujiandaa na mtanange huo, hivyo mchezo huo unatarajia kuwa na upinzani mkali kwa pande zote mbili.

Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya NMB itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Majimaji ya Songea (2-0) mabao yote yakifungwa na kiungo Mudathir Yahya, huku bao pekee lililofungwa na mshambuliaji wa Toto Africans, Wazir Junior, likiizamisha Simba ndani ya Uwanja wa Taifa.
Azam FC itawakosa wachezaji wengine kama kiungo Frank Domayo, Allan Wanga, Racine Diouf, Shomari Kapombe, ambao ni wagonjwa huku Nahodha Msaidizi Himid Mao ‘Ninja’, akiendelea kukosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata wakati timu hiyo ikiichapa Mtibwa Sugar bao 1-0.
Mchezo wa kwanza baina ya hizo katika mzunguko wa kwanza uliisha kwa sare ya mabao 2-2, Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ akifunga mabao yote, wakati Ibrahim Hajibu alifunga ya Simba mabao.
Huo utakuwa mchezo wa 16 kuzikutanisha timu hizo kwenye ligi tangu Azam FC ipande msimu wa 2008/2009, Azam ikishinda nne, Simba saba na kutoka sare mara nne.
picha kutoka maktaba

BAYERN YASHINDWA KUCHUKUA UBINGWA ALLIEN ALLENA
BARCELONA,ATLETICO,REAL MADRID ZOTE ZASHINDA,UBINGWA BADO KAZI
Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao dakika ya 81 ambalo linakuwa la 54 msimu huu katika mchezo wa La Liga dhidi ya Real Betis Uwanja wa Benito Villamarin mjini Sevilla. Barca imeshinda 2-0, bao lingine akifunga Ivan Rakitic ambalo lilikuwa la kwanza dakika ya 50
Nyota wa Real Madrid, Gareth Bale (katikati) akienda hewani dhidi ya mabeki wa Real Sociedad kuifungia bao pekee timu yake katika ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa La Liga leo Uwanja wa Anoeta
source;bin zubery

LICHA YA KUSHINDA BADO FANS WA ARSENAL WAMGANDA WENGER
Ukitegemea shukurani katika mchezo wa soka utakufa na presha. Kocha Arsene Wenger ameifanyia Arsenal mambo mengi sana, ameiingia faida kubwa sana, lakini mashabiki wamemchoka.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England, Arsenal ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Danny Welbeck.
Utaona katika mechi yao dhidi ya Norwich City leo, kuanzia anaingia uwanjani. Mashabiki wakiwa nje walionyesha ujumbe kuwa wamemchoka.
Kama haimchoki, wakati mechi inaendelea, mashabiki waliendelea kumsakama kwa kuonyesha ujumbe unaosisitoza kwamba wamechoka ende zake. WEhhh!
Sources;salehjembe
Subscribe to:
Posts (Atom)