Safu za ushambuliaji za ligi kubwa barani ulaya zinaendelea kuchuana vikali kuelekea mwishoni mwa msimu huu wa 2015/16.

Ronaldo anaongoza kwa kufunga katika chati ya wafungaji bora akiwa na magoli 31 katika mechi 33 akiwa anaitafuta Pichichi yake ya 4 mfululizo, Benzema akiwa na magoli 22 katika mechi 23, Bale amefanikiwa kufunga magoli 16.
BBC wote walifunga katika mchezo dhidi ya Getafe jumamosi hii, wakati goli la Messi la jumapili vs Valencia likawafanya MSN kutimiza magoli 70 kwenye La Liga msimu. Messi akifunga magoli 23 katika mechi 28, Suarez akifunga magoli 36 katika mechi 30 huku Neymar akiwa na magoli 21.
