Sunday, March 13, 2016

BREAKING NEWZ; JPM ATEUA WAKUU WAPYA WA MIKOA.MAKONDA NAE YUMO NDANI;;;


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kati yao 13 ni wapya7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 March, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo
  1. Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga – Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  6. Godfrey Zambi – Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  7. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zelote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  9. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  10. Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  11. Antony Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  12. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  13. Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  14. Jordan Mungire Rugimbana – Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  15. Said Meck Sadick – Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
  16. Magesa Mulongo – Mkuu wa Mkoa Mara.
  17. Amos Gabriel Makalla – Mkuu wa Mkoa Mbeya.
  18. John Vianey Mongella – Mkuu wa Mkoa Mwanza.
  19. Daudi Felix Ntibenda – Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  20. Amina Juma Masenza – Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  21. Joel Nkaya Bendera – Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  22. Halima Omary Dendegu – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
  23. Rehema Nchimbi – Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  24. Mhandisi Evarist Ndikilo – Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
  25. Said Thabit Mwambungu – Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
  26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa – Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU Gerson Msigwa, wakuu wote wa mikoa walioteuliwa wataapishwa Jumanne tarehe 15 March 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Dar es salaam.

SOURCE; MILLARD AYO

AWADH JUMA;GOLI NI ZAWADI KWA MWANANGU KWENYE BIRTHDEI YAKE LEO.......




Kiungo wa simba Awadh juma 'maniche 'amepeleka goli lake kama zawadi kwa mwanaye ambaye leo ni siku yake kuzaliwa na familia yake nzima kwa ujumla.mchezaji huyo aliyeingia dakika ya 70 kuchukua nafasi ya majabv na kufanikiwa kuipa ushindi simba dakika ya 87 kwa shuti kali la nje ya 18 na kuifanya simba kujichiimbia kileleni zaid kw kufikisha point 54



MZEE WA HIRIZI AU POWERBANK UNAMJUAAAAA........

Hirizi ikiwa imetuna hiyo


wachezaji wa Prison wakimvuta ndaw kuwa avue powerbank yake inayochungulia.



picha kutoka maktaba ya salehjembe.


SIMBA ;AMA ZETU AMA ZAO PRISON........LAZIMA TUWAPIGE





Leo katika uwanja wa taifa ligi kuu ya vpl inaendelea katika mechi ya round ya pili kati ya Simba na Prison.katika mechi ya kwanza simnba ilifungwa goli 1-0 na maafande hao wa mbeya.sasa leo ndo marudiano ambao kila timu inataka ushindi Simba ambayo inataka kuongeza gap la point kati yake n Yanga na Azam.na Prison wanatak ushindi kuweza kufika katika  nafasi nzuri katika ligi kuu.inakuwa mechi ya kisasi na prison nd timu ya pili kuifunga Simba kwenye ligi kuu msimuu huu na yanga walioifunga simba mechi zote mbili.


sources;bin zubery na millard ayo