Tuesday, April 19, 2016

SPURS YAIFUNGA STOKE CITY

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane (kushoto) akishangilia na Jan Vertonghen baada ya kuifungia mabao mawili timu yake katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Stoke City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Britannia. Mabao mengine ya Spurs yalifungwa na Dele Alli na sasa timu hiyo inafikisha pointi 68 baada ya kucheza mechi 34 na kuendelea kukaa nafasi ya pili nyuma ya Leicester City yenye pointi 73 za mechi 34 

No comments:

Post a Comment