OSE MOURINHO amepewa uhakika katika masaa 48 yaliyopita kwamba atakuwa kocha mpya wa Manchester United.

Tangu mwezi wa 12 kulikuwepo na taarifa kwamba United wamefanya mawasiliano na Mourinho siku chache baada kocha huyo kufukuzwa Na Chelsea.
Aliambiwa wanamhitaji na asichukue majukumu ya sehemu nyingine.
Tangu wakati huo United wanaripotiwa kumpa mkataba wa miaka 3 wenye thamani ya £60m ambao utamfanya mreno huyo kuwa kocha atakayelipwa zaidi katika historia.
United pia walijaribu kuangalia upatikanaji wa Maurico Pochettino wa Spurs na kocha Paris Saint-Germain Blanc, wakati baadhi ya watu ndani ya klabu walijaribu kutaka Giggs apandishwe cheo.
United pia walijaribu kuangalia upatikanaji wa Maurico Pochettino wa Spurs na kocha Paris Saint-Germain Blanc, wakati baadhi ya watu ndani ya klabu walijaribu kutaka Giggs apandishwe cheo.

United wanafahamu kwamba Mourinho hawezi kukosa ofa nzuri na hii ni nafasi yao ya mwisho kumpata.
SOURCE;SHAFFIHDAUDA
No comments:
Post a Comment