Premier League inatazamwa kama ligi bora ya ndani kama siyo duniani, inajumuisha vilabu vyenye mashabiki wengi kwenye sayari hii. Vilabu kama Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal lakini inabakia kuwa ligi inayotazamwa zaidi na yenye ushindani zaidi ambapo timu yoyote inaweza kufungwa bila kujali inafungwa na timu iliyonafasi gani.
Tangu kuanzishwa kwa Premier League mwaka 1992, ni mameneja saba pekee ambao wameweza kutwaa taji hilo wakiwemo Sir Alex Ferguson, Arsene Wenger na Jose Mourinho.
Lakini kuna mwanaume mwingine ambaye anaweza kuungana na magwiji hao, jinalake ni Claudio Ranieri.
Leicester ya Claudio Ranieri inahitaji pointi tatu pekee ili kutwaa ubingwa wa Premier League, na wanaweza kufanikiwa katika hilo kwa kuifunga Manchester United Jumapili hii.
Ranieri aliteuliwa kuchukua nafasi ya Nigel Pearson wakati wa majira ya joto yaliyopita baada ya kocha huyo wa Kigiriki kupigwa chini na sasa Rarieri yuko mbioni kuwa kocha wa nane kushinda taji la Premier League.
Lakini ma-manager wengine ambao tayari wameshaandika historia zao kwenye kitabu cha makocha waliowahi kushinda Premier League ni hawa wafuatao
7. Carlo Ancelotti-Chelsea-taji 1
Muitaliano huyo mwenye uzoefu alichukua nafasi ya Guus Hiddink mwaka 2009 ambaye alikuwa kocha wa muda. Baada ya miezi miwili pekee ndani ya jiji la London, Ancelotti alinyakua ngao ya jamii ( Community Shield) baada ya kuifunga Manchester United chini ya Sir Alex Furguson kwa mikwaju ya penati kufuatia draw ya 2-2.
He also led the Stamford Bridge outfit to domestic double Premier League and FA Cup titles in his first season at the club.
Alikisaidia kikosi hicho cha Stamford Bridge kutwaa mataji mawili Premier League na FA Cup kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya Chelsea.
Maji aliyoshinda:
- Premier League: 2009–10
6. Kenny Danglish-Blackburn Rovers-taji 1
Kenny Dalglish alikiongoza kikosi cha Blackburn Rovers kushinda kombe la Premier League msimu wa 1994/95, wakimaliza kwa pointi moja mbele ya Manchester United shukrani za pekee zikienda kwa Shearer ns Sutton kwa partnership yao ya hatari.
Shearer na Sutton ni miongoni mwa safu hatari kuwahi kutokea ndani ya Premier League, kwa pamoja wakiwa wamefunga jumla ya magoli 46 (Shearer 31 na Sutton 15) wakiwa wameifungia Blackburn Rovers na kuiwezesha kuchukua ndoo hiyo ya EPL mikononi kwa Manchester United.
5. Manuel Pellegrini-Manchester City-taji 1
Raia huyo wa Chile aliteuliwa kuwa kocha mpya wa Manchester City mwaka 2013 baada ya kuondoka kwa Roberto Mancini, Manuel Pellegrini alikuwa kocha wa kwanza kutoka nje ya Ulaya kushinda Premier League ndani ya msimu wake wa kwanza kwenye dimba la Etihad Stadium.
Roberto Mancini-Manchester City-taji 1
Kocha huyo kutoka Italia alikichukua kikosi cha City kutoka mikononi kwa Mark Hughes kuanzia mwaka 2009 hadi 2011.
Msimu wake wa kwanza, Mancini aliisaidia Man City kumaliza nafasi ya tano, nafasi ya juu kuwahi kushika kabla ya kuiongoza kutwaa taji lao la kwanza mwaka 2012 baada ya miaka 44.
Kikosi cha Mancini ilibidi kipambane kufuta pengo la pointi nane kati yao na Manchester City ndani ya mechi sita za mwisho, kabla ya kutwaa taji hilo dakika za lala salama kwenye mchezo wao wa mwisho kwa magoli yaliyofungwa na Edin Dzeko na Sergio Aguero dhidi ya Queens Park Rangers.
3. Arsena Wenger-Arsenal-mataji 3
Mfaransa huyu alitua Arsenal mwaka 1995, tangu kipindi hicho wakali hao wa London Kaskazini hawajamaliza nje ya nafasi za kucheza Champions League (top four).
Wenger amekiongoza kikosi cha The Gunners kutwaa mataji matatu ya Premier League ndani ya miaka yake 19 aliyodumu lakini ameshindwa kutwaa taji hilo tangu mwaka 2004.
Mataji aliyoshinda:
- Premier League (3): 1997–98, 2001–02, 2003–04
2. Jose Mourinho-Chelsea-mataji 3
Mourinho ameweza kutwaa mataji matatu ya Premier League ndani ya misimu mitano (kwa nyakati mbili tofauti), kwa sasa anatajwa kuwa miongoni mwa ma-kocha bora duniani akiwa ameweza kutwaa mataji ya ndani na vilabu vinne katika nchi nne tofauti.
Tuzungumzie England, Mourinho anashikilia rekodi ndani ya Premier League kama ile ya kuhukua kombe akiwa na pointi nyingi kwenye msimu baada ya kushinda kombe akiwa na pointi 95 mwaka 2004-05.
He also became the most dominant manager in Premier League history last campaign by spending entire season at the top of the table.
Msimu uliopita aliweka rekodi ya kuwa kocha iliyeiongoza Chelsea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa muda mrefu bila kuondolewa.
Mataji aliyoshinda:
- Premier League(3): 2004–05, 2005–06, 2014–15
1. Sir Alex Ferguson-Manchester United-mataji 13
Nyota huyo wa Scotland alitumia miaka 27 akiwa kocha wa Manchester United kati ya 1986 na 2013, akifanikiwa kuweka rekodi ya kushinda mataji 13 ya Premier League na mengine mengi ya ndani pamoja na yale ya Ulaya.
Ferguson alistaafu masuala ya soka mwaka 3013, ni kocha pekee ambaye ameweza kutwaa ubingwa wa Premier League mara tatu mfululizo kati ya 1998/99 na 2000/01 kisha akaruadia tena kati ya 2006/07 and 2008/09.
Mataji aliyowahi kutwaa:
- Premier League (13): 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
No comments:
Post a Comment