
mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates,kati ya arsenal na cryster palace. Timu hizo zimetoka sare ya kufungana 1-1, bao la Arsenal likifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 45 kabla ya Yannick Bolasie kuwasawazishia wageni dakika ya 81

Leonardo Ulloa wa Leicester City akishangilia bao lake la dakika 95 kwa penalti katika sare ya 2-2 na West Ham United jioni ya leo Uwanja wa King Power. Bao lingine la Leicester limefungwa na Jamie Vardy, wakati ya West Ham yamefungwa na Andy Carroll na Aaron Cresswel.

Mshambuliaji Roberto Firmino akishangilia baada ya kuifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 41 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Vitality. Bao lingine la Liverpool limefungwa na Daniel Sturridge wakati la Bournemouth limefungwa na Joshua King
No comments:
Post a Comment