Ubora wa ligi kuu ya Hispania umekuwa unathibitishwa na uwezo unaoneshwa na vilabu vya Real Madrid, Atletico Madrid, Villarreal na Sevilla katika michuano ya bara la ulaya – Champions League na Europa League wiki iliyopita.
Sare ya 0-0 ya Manchester City dhidi ya Los Blancos yanawapa nafasi zaidi vijana wa Zinedine Zidane katika mchezo wa pili wa marudiano utakaofanyika wiki hii kuelekea fainali ya Champions League mnamo May 28. Lakini mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwa upande wa Atletico Madrid ambao watasafiri mpaka Allianz Arena kucheza vs Bayern Munich. Pamoja na kwamba wanaenda Ujerumani na ushindi wa 1-0 shukrani kwa goli la Saul na safu yao nzuri ya ulinzi yenye rekodi bora inaweza kuwasaidia kuvuka.

Ikitokea timu zote za Hispania zikafanikiwa kuingia kwenye fainali za michuano hii mikubwa miwili ya ulaya, oitakuwa ndio mara ya kwanza kwa fainali za michuano hiyo kuhusisha timu za kutoka kwenye ligi moja. Katika historia ya Champions League, kumekuwepo na fainali nne za timu kutoka taifa moja. Hata hivyo, katika misimu hiyo hakujawahi kutokea kukuwepo fainali ya Europa league iliyohusisha timu kutoka taifa moja pia.

sources;shafihdauda
No comments:
Post a Comment