
Hakuna jambo jema kama kuacha kazi mwenyewe kuliko kufukuzwa au kuondolewa. Aliwahi kusema Van Gaal pale alipohusishwa kufukuzwa na Manchester United kupitia tetesi za vyombo vya habari.
Kauli hiyo ya Van Gaal ilikuwa ni mwendelezo wa stori ya Chifu Mkwawa tuliyosoma wakati tupo shule, pale alipoamua kujinyonga kuliko kukamatwa na Wajerumani. Inaonekana alifahamu angekufa kwa mateso makubwa sasa ya nini ateswe wakati uwezo wa kujiondoa mwenyewe anao!? Lakini haikuwa hivyo kwa Mdachi huyo aliyeendelea na kazi yake pale jijini Manchester.
LVG ni mmoja wa makocha wenye misimamo mikali na jambo au kitu anachokisimamia. Hapendi kuyumbishwa au kuendeshwa. Misimamo yake hii ilimfanya kukosana na watu wengi na misimamo yake hiyohiyo ilimpa ushujaa mwingi katika maisha yake. Hiyo ni moja ya sifa ya mwanaume kusimama juu ya kitu anachokiamini. Lakini LVG wa Manchester United ameshindwa kusimama juu ya kauli yake ya kujiondoa mwenyewe kazini hadi pale alipoondolewa. Kama atakuwa anakumbuka maneno yake hayo anaweza akalia kuliko yule Petro aliyemkana Yesu kwa kushindwa kusimama kwenye misimamo yake.
Sidhani kama LVG ataondoka Manchester United kama alivyoingia. Aliingia na matumaini makubwa ya kuisimamisha tena United ambayo ilikuwa imefia mikono mwa David Moyes lakini anaondoka kichwa chini.
Amefeli. Msimu wa kwanza wa LVG ulikuwa wa kuirudisha United katika nafasi nne za juu, alifanikiwa kwa asilimia zote. Msimu wa pili alitakiwa kuifanya United iwe moja ya timu inayogombania makombe na kushinda hususani makombe ya ndani na jukumu la kumaliza nafasi nne za juu ni lazima. Katika msimu wa pili United ameshinda kombe la FA na amemaliza nafasi ya tano. LVG Amefeli tena. Kama van Gaal angeendelea na msimu wa tatu alitakiwa kuifanya kugombania makombe yote atakayoshiriki. Sababu kubwa United kumuondoa LVG ni kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya ni nje ya makubaliano yao ya kwenye mkataba.
Maisha ya LVG yalikuwa magumu Manchester United tangu ile siku ya kwanza waliyocheza na Swansea. Maisha yaliendelea kuwa mabaya zaidi siku waliyocheza na MK Dons hiyo yote ni kutokana na kuibadilisha Manchester United kutoka kwenye staili yao waliyokuwa nayo kwa miaka mingi na kuingiza staili mpya ambayo haijawahi kutumiwa na Manchester United. LVG alileta mfumo mpya wa kumiliki mpira kwa kupiga pasi nyingi lakini mbaya zaidi timu yake ilikuwa inacheza pasi nyingi za kurudi nyuma kuliko kwenda mbele.
Tangu yupo Ajax LVG ni muumini mkubwa wa mpira wa pasi lakini tofauti na huku Manchester United timu zake zilikuwa zinafunga magoli ya kutosha na kuruhusu machache. Jambo bora la LVG kwa timu ya United ni muendelezo wake wa kutoa nafasi kwa vijana ambao wanazalishwa na timu hiyo pia kufanya usajili wa wachezaji wenye umri wa wastani kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu.
Wakati vyombo vya habari vikijaribu kuukosoa mfumo wa LvG katika timu ya Manchester United alijitetea kwa kusema “It’s a process. My philosophy needs time” akimaanisha “Ni mchakato, falsafa yangu inahitaji muda”. Hata Roma haikujengwa kwa siku moja, binafsi niliamini Van Gaal angeutumia msimu wake wa kwanza kuisoma ligi ya England na kisha msimu wa pili kurudi akiwa amejipanga sawia kupambana na wapinzani lakini bado alisimamia msemo wa falsafa zake ambazo zinahitaji muda zaidi, timu kama United ni timu inayojiendesha kibiashara zaidi kutegemea mikataba ya wadhamini mbalimbali duniani pamoja na kuwa na mashabiki wengi duniani lakini kukosa kushiriki michuano mikubwa ya Ulaya ni kuisababishia timu hasara.
Van Gaal kaacha mambo mengi ya kukumbukwa hasa katika usajili wa Tony Martial ambaye amegeuka kuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo. Kila alichofanya kiligeuka kuwa kinyesi hakiwavutia mashabiki zaidi ya wapinzani ambao walikuwa wanafurahi anguko la United. Katika kazi ya ukocha ya LVG hii hatoweza kuisahau. It’s a process. It’s philosoph
source shaffihdauda.
No comments:
Post a Comment