Ubora wa ligi kuu ya Hispania umekuwa unathibitishwa na uwezo unaoneshwa na vilabu vya Real Madrid, Atletico Madrid, Villarreal na Sevilla katika michuano ya bara la ulaya – Champions League na Europa League wiki iliyopita.
Sare ya 0-0 ya Manchester City dhidi ya Los Blancos yanawapa nafasi zaidi vijana wa Zinedine Zidane katika mchezo wa pili wa marudiano utakaofanyika wiki hii kuelekea fainali ya Champions League mnamo May 28. Lakini mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwa upande wa Atletico Madrid ambao watasafiri mpaka Allianz Arena kucheza vs Bayern Munich. Pamoja na kwamba wanaenda Ujerumani na ushindi wa 1-0 shukrani kwa goli la Saul na safu yao nzuri ya ulinzi yenye rekodi bora inaweza kuwasaidia kuvuka.
Ikitokea timu zote za Hispania zikafanikiwa kuingia kwenye fainali za michuano hii mikubwa miwili ya ulaya, oitakuwa ndio mara ya kwanza kwa fainali za michuano hiyo kuhusisha timu za kutoka kwenye ligi moja. Katika historia ya Champions League, kumekuwepo na fainali nne za timu kutoka taifa moja. Hata hivyo, katika misimu hiyo hakujawahi kutokea kukuwepo fainali ya Europa league iliyohusisha timu kutoka taifa moja pia.
Namba ya juu zaidi ya idadi ya timu katika fainali za UCL na Europa ni timu tatu, jambo hilo lilitokea, msimu wa 1989-90, 1994-96 na 1997-98 wakati vilabu vitatu kutoka Italia vilipokutana kwenye fainali zote mbili. Vilabu vitatu vya Ujerumani navyo vimewahi kuingia katika fainali hizo mbili kwa pamoja msimu wa 1979-80, wakati msimu wa 2013-14, vilabu vitatu vya Spain vilicheza kwenye fainali hizo mbili za michuano ya ngazi ya juu ya ulaya.
sources;shafihdauda

No comments:
Post a Comment